UVCCM SHINYANGA MJINI NA ZIARA YA MAMA FULL BOX OPARESHENI

UVCCM SHYMJINI NA ZIARA MAMA FULL BOX OPARESHENI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Shinyanga Mjini,umeendelea na ziara ya Kata kwa Kata ya kuhamasisha vijana, wanachama wa chama hicho na wananchi,kuwa wajiandae kwenye uchaguzi mkuu 2025, pamoja na kumpigia kura nyingi Rais Samia Suluhu Hassan na wagombea wote wa CCM.
Ziara hiyo imeanza jana ambayo ina kauli mbiu isemayo "Mama Full Box Oparesheni" ikiwa na maana kura za Rais Samia zijae kwenye Saduku la kura siku hiyo ya uchaguzi, ili apate ushindi wa kishindo na kuendelea kuwatumikia Watanzania na kuwaletea maendeleo.

Mwenyekiti wa umoja huo Abdulazizi Sakala,akizungumza leo Aprili 6,2025 mara baada ya kumaliza kuzindua Shina la Mama Kata ya Mwawaza, amesema wao vijana wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini,wanaunga Azimio la Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, la kumpitisha Rais Samia kuwa ndiye atagombea uchaguzi Mkuu 2025 kupitia Chama hicho, pamoja na Dk. Emmanuel Nchimbi kuwa Makamu wake.
Amesema kutokana na kuunga mkono Azimio hilo,wameamua kufanya ziara ya kuhamasisha vijana, wanaCCM na wananchi wajiandae na uchaguzi mkuu, na kuhakikisha wanampigia kura nyingi Rais Samia kwa kujaza Sanduku la kura ili apate ushindi wa kishindo,kutoka na mambo makubwa ya kimaendeleo ambayo ameyafanya kwenye utawala wake.

"UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, tumeridhishwa na kazi kubwa ambayo ameifanya Rais wetu Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea maendeleo Watanzania, na sisi tumeamua kufanya ziara ya kuhakikisha kura za Rais Samia zinajaa kwenye Sanduku la kura siku ya uchaguzi maarufu"Mama Full Box Oparasheni,"amesema Sakala.
Aidha,ametolea mfano katika Kata hiyo ya Mwawaza mambo makubwa ambayo ameyafanya Rais Samia, kuwa ni kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga,ambayo ipo eneo hilo la Mwawaza,na sasa ana kwenda kujenga Barabara ya Hospitali hiyo kwa kiwango cha Lami.

Naye Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula,amewatoa hofu wananchi wapuuze maeneo ya kwamba uchaguzi hautakuwepo, na kueleza kwamba uchaguzi upo pale pale,na watakao susa wasuse, bali siku hiyo ya uchaguzi wajitokeze kwa wingi na kuwapigia kura wagombea wote wa CCM Wabunge,Madiwani na Rais Samia.
Pia,amewasihi Wanachama wa Chama hicho kwamba kipenga cha kuchukua fomu kitakapo tangazwa cha nafasi ya Udiwani na Ubunge,wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu na kugombea nafasi hizo kwa kujipima kwanza kama wanatosha kwenye nafasi hizo.

Katika ziara hiyo ya Mama Full Box Operation ina ambatana pia na uzinduzi wa Mashina ya Mama".

TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizungumza.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizungumza.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akikabidhiwa Bendera ya Chama.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akiwasilia kuzindua Shina la Mama Kata ya Mwawaza.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizindua Shina la Mama Kata ya Mwawaza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464