UVCCM (W) SHINYANGA MJINI YAKOSHWA NA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KATA YA IBADAKULI

UVCCM (W) SHINYANGA MJINI YAKOSHWA NA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KATA YA IBADAKULI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Shinyanga Mjini,wameeleza kuridhishwa na kazi kubwa ambayo ameifanya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa asilimia100 katika Kata ya Ibadakuli.
Wamesema miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa kwenye Kata hiyo, ukiwamo mradi mkubwa wa kimkakati ambao ni ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Shinyanga, ambao upo kwenye eneo la Kata hiyo.

Hayo yamebainishwa leo Aprili 7,2025 na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala,wakati alipowasili kwenye Kata hiyo kuzindua Shina la Mama,pamoja na kuzungumza na Vijana,Wananchi na WanaCCM,katika ziara ya UVCCM"Mama Full Box Oparesheni".
"UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini tumeridhishwa na kazi kubwa ambayo anaifanya Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan, ya utekelezaji wa ilani ya CCM pamoja na kuwaletea maendeleo wananchi," amesema Sakala.

Amesema kutokana na kazi kubwa ambayo ameifanya Rais Samia ya kuwaletea maendeleo wananchi ndani ya miaka yake minne ya utawala wake,wao kama vijana,wameamua kuja na kampeni ya Mama Full Box Oparesheni ikiwa lengo la kuhamasisha wananchi wajiandae na uchaguzi mkuu 2025, pamoja na kumpigia kura nyingi Rais Samia na kujaza Sanduku la kura siku ya uchaguzi,ili ashinde kwa kishindo.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula, amesema Rais Samia amefanya mambo makubwa hapa nchini, pamoja na kuikamilisha miradi ya kimkakati ambayo iliachwa na Hayati Rais John Pombe Magufuli ukiwamo uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Shinyanga.

Amesema Uwanja huo wa Ndege nikichocheo kikubwa cha uchumi wa mkoa wa Shinyanga na Taifabkwa ujumla ,pamoja na uboreshwaji wa huduma za jamii katika Kata hiyo ya Ibadakuli.
Katika hatua nyingine,amewataka Watanzania wajiandae na uchaguzi mkuu 2025, kwamba hakuna ambaye anaweza kuzuia uchaguzi huo, sababu ni takwa la kikatiba.

ziara hiyo ya UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini ya "Mama Full Box Oparesheni" leo ipo katika Kata ya Ibadakuli na Kolandoto,yenye kauli mbiu isemayo 2025# Kazi na Utu,Tunasonga Mbele.

TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizungumza.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizungumza.
Diwani wa Vitimaalumu Zuhura Waziri akizungumza.
Mjumbe wa Kamati ya utekezaji wilaya ya Shinyanga Mjini Halima Issa akizungumza.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abudalaziz Sakala akizundua Shina la Mama Kata ya Ibadakuli.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464