UVCCM (W)SHINYANGA MJINI YAWATAKA VIJANA WASITUMIKE VIBAYA KISIASA KUVURUGA UCHAGUZI MKUU 2025
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Shinyanga Mjini,umewataka vijana wasitumike vibaya kisiasa kuvuruga uchaguzi mkuu 2025.
Wamesema kuna moja ya Chama cha upinzani,kimepanga kuvuruga uchaguzi huo,wakisema hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi "No Reform No Election".
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula,amebainisha hayo leo Aprili 8,2025 mara baada ya Mwenyekiti wa Umoja huo Abdulaziz Sakala, kumaliza kuzindua Shina la Mama Kata ya Chamaguha,katika ziara yao ya Mama Full Box Oparesheni.
Amewataka wananchi kwamba wajiandae na uchaguzi Mkuu 2025, sababu utakuwapo kwa mujibu wa Katiba,na kwamba hauwezi kuhairishwa kwa matakwa ya chama chochote kile,huku akiwasihi vijana wasikubali kutumika kuvuruga uchaguzi huo.
"Kuna chama kimoja kimepanga kuvuruga uchaguzi mkuu 2025 wakisema 'No Reform No Election' yani hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi, na kunatetesi kwamba siku ya uchaguzi watafanya maandamano,ni waombe tu vijana msikubali kutumika vibaya kuvuruga uchaguzi huo,"amesema Katalambula.
"Wananchi uchaguzi mkuu utakuwepo kwa mujibu wa Katiba,na hawa wapinzani wameona hawana hoja kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo kwa wananchi,ndiyo maana wanataka kukimbia mechi kwa kisingizio cha No Reform No Election," ameongeza.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala,amesema kwamba katika uchaguzi huo, CCM watashinda kwa kishindo sababu miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa kwa wananchi chini ya Rais Samia.
Aidha, amesisitiza suala la Amani katika uchaguzi huo,na kueleza kwamba nchi ambayo haina Amani haiwezi kupiga hatua kimaendeleo.
Ziara hiyo ya UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini imelenga kuzindua Mashina ya Mama katika Kata zote 17 za Manispaa ya Shinyanga, pamoja na kuhamasiha wananchi wajiandae na uchaguzi mkuu,sababu utakuwepo.
TAZAMA PICHA 👇👇
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulazizi Sakala akizungumza.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizungumza.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizindua Shina la Mama Kata ya Chamaguha.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464