UVCCM (W)SHINYANGA MJINI BEGA KWA BEGA NA RAIS SAMIA ZIARA YA MAMA FULL BOX OPARESHENI

UVCCM (W)SHINYANGA MJINI BEGA KWA BEGA NA RAIS SAMIA ZIARA YA MAMA FULL BOX OPARESHENI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini,wameendelea na ziara ya Mama Full Box Oparesheni,kwa kuzungumza na wananchi wajiandae na uchaguzi mkuu 2025, huku wakizindua Mashina ya Mama.
Leo Aprili 9,2025 wamefanya ziara katika Kata ya Lubaga kwa kuzungumza na wananchi pamoja na kuzindua Shina la Mama kwenye Kata hiyo.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Abdulaziz Sakala, amewaambia wananchi kwamba wajiandae na uchaguzi mkuu sababu utakuwepo na hakuna chama chochote kinachoweza kuzuia uchaguzi huo sababu ni takwa la Kikatiba.
Amesema CCM imeshajipanga kushiriki kwenye uchaguzi huo, na tayari wameshampitisha Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa ndiye atagombea Urais kwa tiketi ya CCM.

“CCM tutashinda kwenye uchaguzi mkuu, sababu Rais wetu Samia ameupiga mwingi na kutekelezwa miradi mingi ikiwamo ya kimkakati,”amesema Sakala.
Aidha, amemwagia sifa Rais Samia kuwa anatosha kuendelea kutawala katika nchi yetu sababu ni Rais ambaye amefanya mambo makubwa licha ya kupokea nchi katika wakati mgumu kwa kuondokewa na Hayati Rais John Pombe Magufuli, pamoja na nyakati ngumu za ugonjwa wa Corona, lakini amesimama na kila kitu kimekwenda sawa.

Amesema pia Rais Samia ameimarisha demokrasia hapa nchini, na hata kuruhusu mikutano ya hadhara,pamoja na baadhi ya wanasiasa waliokimbia nchi wamerejea nyumbani.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula, amesema Rais Samia yupo kwa ajili ya maslahi ya Watanzania, na amekamilisha miradi mingi ya maendeleo ukiwamo ya kimkakati,ujenzi wa Reli ya SGR,Bwawa la Mwalimu Nyerere,Daraja la Busisi,Ujenzi Uwanja wa Ndege Ibadakuli Shinyanga.

Diwani wa Lubaga Rubeni Dotto, amesema katika Kata hiyo haijawahi kutokea kupokea fedha nyingi za miradi ya maendeleo, na kwamba ndani ya Utawala wa Rais Samia wamepokea zaidi ya sh.bilioni Moja,pamoja na kujengwa Shule mpya ya Sekondari za Zahanati huduma ambazo hazikuwepo kwenye Kata hiyo.

TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizungumza.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizungumza.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya utekelezaji UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Halima Issa akizungumza.
Katibu Hamasa na Chipukizi UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Samson Suleiman akizungumza.
Diwani wa Lubaga Rubeni Dotto akizungumza.
Uzinduzi wa Shila la Mama Kata ya Lubaga ukiendelea.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akipandisha Bendera.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464