UVCCM (W)SHINYANGA MJINI WATOA WITO WA AMANI NA UTULIVU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025,WASISITIZA USHIRIKI WA DEMOKRASIA NA HESHIMA YA KATIBA
JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini,wametoa wito kwa Watanzania,kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025,waufanye kwa amani na utulivu.
Hayo yamebainishwa leo Aprili 11,2025 na Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini Naibu Katalambula, wakati akizungumza na wananchi wa Ndembezi,mara baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Abdulaziz Sakala kumaliza kuzindua Shina la Mama Kata ya Ndembezi.
Amesema kwa vyama ambavyo havitaki kushiriki uchaguzi mkuu 2025, ni vyema wakajitoa kwa hiari yao, na siyo kutaka kuvuruga uchaguzi huo na kuharibu amani ya nchi,sababu suala la uchaguzi siyo matakwa ya chama chochote bali lipo kikatiba.
"Nawaombeni sana Watanzania uchaguzi mkuu wa mwaka huu, tuufanye kwa amani na utulivu,na wasio taka kushiriki uchaguzi waache kwa hiari yao na siyo kutaka kuvuruga amani ya nchi sababu kufanya uchaguzi ni takwa la kikatiba," amesema Katalambula.
Amesema CCM tayari wao wameshajipanga kushiriki kwenye uchaguzi mkuu, ambapo wameshampitisha Rais Samia Suluhu Hassani kuwa ndiye mgombea pekee wa Urais kwa tiketi ya CCM, na jana wameshatangaza zoezi la uchukuaji fomu kugombea nafasi za Udiwani na Ubunge kuanzia mwezi Mei.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala, amesema katika uchaguzi huo mkuu ambao utafanyika Oktoba mwaka huu, kwamba CCM wana kwenda kushinda kwa kishindo kwa nafasi zote za Udiwani,Ubunge na Rais.
Amesema dalili za ushindi huo tayari zimeshaonekana, kutokana na mambo makubwa ya kimaendeleo ambayo ameyafanya Rais Samia kwa Watanzania,pamoja na kuikamilisha miradi ya kimkakati ukiwamo ujenzi wa Reli ya kisasa SGR,Bwawa la Mwalimu Nyerere,Daraja la Busisi,na kwa Shinyanga ujenzi wa Uwanja wa Ndege uliopo Ibadakuli.
Amesema wao vijana wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, baada ya kuona maendeleo makubwa ambayo yamefanywa na Rais Samia,wakaona ni vyema wafanye ziara ya Mama Full Box Oparesheni, ili kuwa andaa wananchi kushiriki uchaguzi mkuu,pamoja na kumpigia kura nyingi za ushindi Rais Samia siku hiyo ya uchaguzi.
Ziara hiyo ya Mama Full Box Oparesheni, ina kauli mbiu isemayo, Kazi na Utu,Tunasonga Mbele.
TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizungumza.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizungumza.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akiwa na Hashimu Issa.
Diwani wa Ndembezi Victor Mmanywa akizungumza.
Katibu wa CCM Kata ya Ndembezi Pendo Sawa akizungumza.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Halima Issa akizungumza.
Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Samson Suleiman akizungumza.
Uzinduzi wa Shina la Mama Kata ya Ndembezi ukiendelea.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akipanda Mti.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464