CHADEMA KANDA YA SERENGETI WAPIGILIA MSUMARI KAULI YA "NO REFORMS,NO ELECTION" UCHAGUZI MKUU 2025

CHADEMA KANDA YA SERENGETI WAPIGILIA MSUMARI KAULI YA "NO REFORMS,NO ELECTION" UCHAGUZI MKUU 2025

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Serengeti kinachojumuisha mikoa ya Mara, Simiyu, na Shinyanga, kimeunga mkono msimamo wa Makao Makuu ya chama hicho kwamba hawatashiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 iwapo hakutakuwa na mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi nchini “No Reforms, No Election.”
Hayo yamebainishwa leo Aprili 16,2025 na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti Lucas Ngoto, wakati akitoa tamko lao kwa waandishi wa habari,kikao kichofanyika Mjini Shinyanga.

Amesema uchaguzi ni Takwa la Kikatiba,ambapo wananchi wanapaswa kuchagua viongozi ambao wanawataka, lakini Katiba hiyo imekuwa ikikeukwa hasa Ibara ya 8, na uchaguzi kufanyika ndivyo sivyo, na ndiyo maana wanataka mabadiliko ya uchaguzi, ili uwe huru na haki na kupatikana wagombea kihalali na siyo kwa dhuruma.
Ngoto ametolea mfano wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwaka 2024, akidai kuwa ulikumbwa na kasoro nyingi, zikiwemo wagombea wao kuenguliwa kwa pingamizi zisizo na msingi, na baadhi ya walioshinda kushindwa kuapishwa.

“Kutokana na matukio ya dhuruma yaliyotokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita, tunatambua kuwa iwapo hatutachukua tahadhari, hali hiyo itajirudia kwenye Uchaguzi Mkuu 2025, Hivyo, tunasimama na viongozi wetu wa kitaifa kusema wazi: No Reforms, No Election,”amesema Ngoto.
Aidha,wameimeitaka Serikali kumuachia huru Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Tundu Lissu, wakidai kwamba kesi ya uhaini inayomkabili ni jaribio la kuwakwamisha kisiasa, na Chama Tawala kuhofia uchaguzi

“Serikali isitake kututoa kwenye ajenda yetu ya kudai mabadiliko kwa kumkamata Lissu, kwa sasa tunazo ajenda mbili: No Reforms, No Election na Free Tundu Lissu,” ameongeza.
Kwa upande mwingine,Ngoto amefafanua kuwa uamuzi wa kutosaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi haumaanishi kuwa CHADEMA imeshindwa kushiriki uchaguzi, kwa kuwa hakuna sheria inayowazuia kushiriki uchaguzi kwa msingi huo.

Naye Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Simiyu, Mussa Onesmo, amelaani kukamatwa kwa Tundu Lissu, na kutangaza kuwa wataandaa msafara wa wanachama zaidi ya 100 kwenda Dar es Salaam kushinikiza kuachiliwa kwake.

TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti Lucas Ngoto akizungumza.
Katibu wa Chadema Kanda ya Serengeti Jackson Mnyawami akizungumza.
Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Shinyanga Titus Jilungu akizungumza.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Simiyu Mussa Onesmo akizungumza.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara Chacha Heche akizungumza.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara Chacha Heche (kulia)akikabidhi Ripoti ya Madhira uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita kwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti Lucas Ngoto.
Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano wa Chadema Kanda ya Serengeti.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464