SIMBA SC TUMEVUKA,MNYAMA AUNGURUMA

TIMU YA SIMBA SC IMEVUKA KUFUZU HATUA YA NUSU FAINALI BAADA YA KUIONDOSHA TIMU YA AL MASRY KWA MIKWAJU YA PENATI.

Katika Mchezo huo uliochezwa Dimba na Mkapa Simba hadi wanamaliza Dakika 90 walikuwa wameshinda Magoli 2-0, na Machezo uliochezwa ugenini Simba walifungwa Goli 2-0 ,ambapo Timu Moja inatakiwa iende Nusu Fainal ndipo ikapigwa Mikwaju ya Penati.

Mabao ya Simba yamefungwa na Elie Mpanzu pamoja na mshambuliaji matata Steven Mukwala, ambao waliweka uhai mpya kwenye mchezo huo kwa kusawazisha jumla ya mabao katika dakika muhimu.

Hatua ya penalti ikaamua hatma ya mchezo, ambapo walinda mlango na wapigaji wa Simba walionesha utulivu na umahiri wa hali ya juu, na hatimaye kutinga Nusu Fainali kwa kishindo.

Katika hatua inayofuata, Simba SC itakutana na mshindi kati ya Zamalek ya Misri dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini – mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka ndani na nje ya Tanzania.

Kufuatia ushindi huo wa kihistoria, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa salamu za pongezi kwa wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki wa Simba.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464