Hata biashara nazo zinahitaji ulinzi
Kwa miaka mingi nimekuwa nikifanya biashara maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam, nashukuru kipato ambacho nimekuwa nikipata kinaniwezesha kumudu gharama za maisha ya kila siku.

Naweza kuitunza familia vizuri, kusomesha watoto wangu, kuwasaidia wazazi wangu na kufanya mambo mengine ya kimaendeleo kama kujenga na kununua mashamba kwa ajili ya uwekezaji wa hapo baadaye.