PAPA FRANCIS AFARIKI DUNIA

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, amefariki dunia leo Aprili 21,2025 kwenye Jumatatu ya Pasaka akiwa na umri wa miaka 88 ambapo Vatican imethibitisha na kusema Papa amefariki akiwa kwenye makazi yake katika Casa Santa Marta, Vatican
Papa ambaye alizaliwa mwaka 1936 hivi karibuni amepitia changamoto ya upumuaji hadi kuhitaji mashine ya kusaidia kupumua na amekuwa akikabiliwa na matatizo ya kiafya ikiwemo maambukizi ya mapafu(nimonia) hadi kupelekea kulazwa kwa wiki kadhaa kabla ya baadaye afya yake kuimarika.