UVCCM (W)SHINYANGA MJINI YAWATAKA VIJANA WAWE WAZALENDO NA NCHI YAO,ZIARA YA MAMA FULL BOX OPARESHENI


UVCCM (W)SHINYANGA MJINI YAWATAKA VIJANA WAWE WAZALENDO NA NCHI YAO,ZIARA YA MAMA FULL BOX OPARESHENI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga mjini,wamewataka vijana kote nchi wawe wazalendo na nchi yao, ili kuilinda amani iliyopo na wasikubali kutumiwa na wanasiasa kuivuruga.
Hayo yamebainishwa leo Aprili 10,2025 na Jumuiya hiyo wakati wakizindua Mashina ya Mama Kata ya Masekelo na Ndala,pamoja na kuzungumza na wananchi na wana CCM kwenye mikutano, ili kuwahamasisha wajiandae na uchaguzi mkuu 2025.

Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Samson Suleiman,amesema uzalendo ni kitu muhimu katika kuilinda amani ya nchi, na kuwasihi vijana kwamba wasikubali kutumika na baadhi ya wanasiasa kuichafua Amani, ambayo imelindwa na viongozi kwa nguvu zote.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula,amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha demokrasia hapa nchini,huku akivisihi vyama vya siasa kuitumia vizuri demokrasia hiyo, na siyo kutaka kuvuruga amani ya nchi.

Aidha, amesema katika uchaguzi mkuu (2025), CCM wanakwenda kushinda kwa kishindo kwenya nafasi zote za Udiwani,Ubunge na Rais,kutokana na kazi kubwa ambayo imefanywa ya utekelezwaji wa miradi ya maendeleo, ikiwamo kukamilishwa miradi ya kimkakati chini ya Rais Samia.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala, amempongeza Rais Samia kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa asilimia 100, tena kwa vitendo na kwamba kila mtu anajionea kwa macho mambo makubwa ambayo ameyafanya ya kimaendeleo hapa nchini.

Amesema kutokana na utekelezaji huo wa Ilani ya CCM kwa asilimia 100,wao kama UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, ndipo wakaamua kufanya ziara Mama Full Box Oparesheni, ili kuitangaza miradi hiyo kwa wananchi, na kuwahamasisha wajiandae na uchaguzi mkuu,pamoja na siku hiyo ya uchaguzi mwezi Oktoba, wampigie kura nyingi za ushindi Rais Samia na ashinde kwa kishindo.
Katika ziara hiyo ulifanyika pia uzinduzi wa Ofisi ya UVCCM Kata ya Ndala,pamoja na kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wanafaunzi wenye uhitaji katika shule ya Msingi Ndala.

Ziara hiyo ya Mama Full Box Oparesheni,ina kauli Mbiu isemayo, Kazi na Utu, Tunasonga Mbele, ambapo kesho watakuwa Kata ya Mjini na Ndembezi.

TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti w UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizungumza.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizungumza.
Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Halima Issa akizungumza.
Katibu Hamasa na Chipukizi UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Samson Suleiman akizungumza.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akikata Utepe kuzindua Shina la Mama Kata ya Masekelo.
Uzinduzi Shina la Mama Kata ya Masekelo ukiendelea.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akipandisha Bendera katika Shina la Mama Kata ya Masekelo.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akisalimiana na Diwani wa Masekelo Peter Koliba.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizindua Shila la Mama Kata ya Ndala.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akikata Utepe kuzindua ofisi ya UVCCM Kata ya Ndala.
Diwani wa Kata ya Ndala Zamda Shabani akiongea.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala, akikabidhiwa Bendera ya Chama,katika ziara ya Mama Full Box Oparesheni.
UVCCM wakikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa wanafunzi wenye uhitaji katika shule ya Msingi Ndala.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464