Dawa ya mume mwenye gubu ndani ya nyumba!
Ndoa ama mahusiano bila ya mapenzi huwa si hayaendi mbali kwani mapenzi huwa kiini cha umoja na mshikamano. Wapenzi kwenye mahusiano hupaswa kuwajibika na kuelewana kwa wakati wowote ili kuwezesha mahusiano kuwa yenye matamanio.

Tulikuwa tumefunga ndoa na mume wangu ambapo mwaka mmoja ulikuwa umepita sasa tangu kufanya harusi, kwa hakika maisha yalikuwa mazuri kwani Ben ambaye ndiye mume wangu alikuwa mwenye mapenzi na mtu ambaye alikuwa mchangamfu katika kila hali.