MWENYEKITI CCM NYANG’HWALE AWAPA MAUA YAO UVCCM(W)SHINYANGA MJINI KUMSEMEA VIZURI RAIS SAMIA,ZIARA YA MAMA FULL BOX OPARESHENI

MWENYEKITI CCM NYANG’HWALE AWAPA MAUA YAO UVCCM(W)SHINYANGA MJINI KUMSEMEA VIZURI RAIS SAMIA,ZIARA YA MAMA FULL BOX OPARESHENI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Nyang’hwale Alhaji Adamu Mtole, ameipongeza Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini,kwa kufanya ziara na kumsemea vizuri Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, pamoja na kuitangaza miradi ya maendeleo ikiwamo ya kimkakati ambayo ameitekeleza kwa wananchi.
Amebainisha hayo leo Aprili 8,2025, wakati UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini walipokuwa wakizungumza na wananchi wa Kizumbi kwenye mkutano wa hadhara,pamoja na kuzindua Shina la Mama Kata ya Kizumbi.

Amesema yeye alikuwa safari akitokea Mwanza kwenda Kahama, lakini alipoona nguo za kijani kwenye mkutano huo ilibidi asimame, na aliposikiliza nini kinaongelewa ameguswa sana na kusikia vijana hao wakimsemea vizuri Rais Samia, pamoja kuitangaza miradi ambayo ameitekeleza ikiwamo ya kimkakati.
“Nawapongeza sana UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini kwa msehemea vizuri Rais Samia, ambapo ndani ya Utawala wake wa miaka Minne amefanya mambo makubwa utafikili ni miaka 10,”amesema Alhaji Adamu.

“kutokana na kazi kubwa ambayo ameifanya Rais Samia,mimi nikiwa miongoni mwa wajumbe wa mkutano mkuu, ambapo tupo wajumbe 1,928 lakini ndani ya mkutano siku ambayo tunampitisha Rais Samia kuwa ndiye atakuwa Mgombea pekee wa Urais kwa tiketi ya CCM tulikuwa 1,924, na wote tulimpigia kura za ndiyo, yote hii ni kutokana na namna alivyochapa kazi na tunamhitaji tena,”ameongeza.
Diwani wa Kizumbi Ruben Kitinya,naye amempongeza Mwenyekiti huyo wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala, kwamba aliichukua Jumuiya hiyo ikiwa imeyumba, lakini kwa busara zake sasa hivi imetulia na vijana wamekuwa na nidhamu,huku akimsihi aendelee kuchapa kazi ya kukisemea vizuri Chama.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Abdulaziz Sakala, amesema wao wameamua kufanya ziara ya Mama Full Box Oparesheni, kwa ajili ya kuwahamasisha wananchi wajiandae na uchaguzi mkuu 2025, kufungua Mashina ya Mama,kuisemea miradi ikiwamo ya kimkakati ambayo imetekelezwa na Rais Samia,pamoja na kumpigia kura nyingi za ushindi wa kishindo siku ya uchaguzi mkuu.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula, amesema wao vijana wanaungana na Azimio la Mkutano Mkuu kumpitisha Rais Samia kuwa ndiye Mgombea pekee wa Urais uchaguzi mkuu 2025 kwa tiketi ya CCM, na wameridhishwa na kasi ya utendaji wake kazi.

Aidha, amewataka wananchi wajiandae na uchaguzi mkuu, na kupuuza maeneo ya Chama kimoja cha upinzani ambacho kinasema “no reform na no election” na kueleza kwamba hakuna chama chochote kinachoweza kuzuia uchaguzi, sababu suala hilo lipo kwa mujibu wa Katiba.

TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyan'ghwale Alhaj Adamu Mtole akizungumza.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nyang'hwale Kaswahili Enock akizungumza.
Diwani wa Kizumbi Rubeni Kitinya akizungumza.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizungumza.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizungumza.
Katibu Hamasa na Chipukizi Samson Suleiman akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyang'hwale Alhaji Adamu Mtole (kushoto)akiwa na Mwenyekiti w UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala, wakifurahia jambo.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyang'hwale Alhaji Adamu Mtole (kushoto)akiwa na Mwenyekiti w UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala,wakifurahia jambo.
Uzinduzi wa Shina la Mama Kata ya Kizumbi ukiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464