MILION 255.8 ZATOLEWA KWA VIKUNDI 19 VYA WANAWAKE, VIJANA, NA WATU WENYE ULEMAVU MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga MC
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga katika kuhakikisha jamii inaondokana na umasikini, imetoa mikopo ya asilimia 10 isiyo na riba, mikopo inayotolewa kupitia makusanyo ya ndani ya halmashauri kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Akikabidhi mikopo hiyo mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika leo aprili 02, 2025 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga wakili julius mtatiro amewasihi wanufaika hao kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili iweze kunufaisha vikundi vingine
"Uchukuaji wa mikopo ni hiali, lakini urejeshaji wa mikopo ni lazima na kwa wakati, Mkurugenzi wetu chini ya watendaji wake wamefanya kila kitu Kuhakikisha jamii na wakazi wa manispaa wanaondokana na umasikini ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali kuu, fedha hizi zitumike kama mlivyoandika kwenye maandiko yenu ya Miradi, rejesheni kwa wakati, ili wadogo zenu, ndugu zenu, wanashinyanga nao waweze kupata mikopo hii.” Wakili Mtatiro.
Akitoa Elimu juu ya namna ya kupata mikopo ya asilimia kumi Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Nyanjula Kiyenze amesema kigezo kikubwa cha kupata mkopo huo wa asilimia 10 ni kikundi cha watu kuanzia watano kwa vikundi vya wanawake na vijana huku watu wenye ulemavu anaruhusiwa kukopa mkopo huo hata mtu mmoja.
Kwa upande wake Msitahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias R. Masumbuko amesema mpaka sasa kwa mwaka fedha 2024/2025 mikopo hiI imetolewa kwa awamu mbili ambapo awali ilitolewa jumla ya milioni 90,000,000 Kwa vikundi vitatu, huku kwa awamu hii ya pili jumla ya Milioni 255,879,500 imetolewa kwa jumla ya vikundi 19 kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya Shinyanga
Penina Ezekiel, Razalo John na Isack Samwel ni baadha ya wanufaika wa mikopo hii wameishukuru serikali kuleta mikopo hii inayowasaidia kuondokana na mikopo kandamizi kama kausha damu sambamba na kuwaepusha kuwa Ombaomba, Kupunguza wimbi la vijana wasio na Ajira, huku wakisema mikopo hiyo huku wakiahidi kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili iweze niwanufaisha vikundi vingine.
TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utoaji wa mikopo.
Mstahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utoaji wa mikopo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga Nyanjura Kiyenze akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utoaji wa mikopo.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Ndg. Peres Kamugisha akiwasilisha taarifa ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akikabidhi hundi ya Shilingi Milioni 255.
Diwani wa kata ya Mjini Mhe. Gulamhafeez Mukadam akizungumza wakati wa gafla hiyo ya utoaji mikopo.
Pikipiki za mkopo zilizotolewa na manispaa ya Shinyanga kwa vijana.
Pikipiki za mkopo zilizotolewa na manispaa ya Shinyanga kwa vijana.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia hafla hiyo ya utoaji mikopo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464