TASAF YAJIVUNIA MAFANIKO KAYA MASKINI KUZIINUA KIUCHUMI

TASAF YAJIVUNIA MAFANIKO KAYA MASKINI KUZIINUA KIUCHUMI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MFUKO wa Maendeleo ya Jamii TASAF, kupitia mpango wa kunusuru Kaya Maskini,umeeleza kufanikiwa kuziinua kiuchumi Kaya maskini.
Hayo yamebainishwa leo Aprili 5,2025 na Afisa Habari na Mawasiliano kutoka TASAF Christopher Kidanka, wakati akiwasilisha taarifa ya TASAF kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga.

Amesema mfuko huo ulianzishwa mwaka 2000 kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii,kwa kutoa Ruzuku za msingi kwenye Kaya maskini, na kwamba mpaka sasa Kaya nyingi zimeondokana na umaskini, na zingine kuondolewa kwenye mpango huo mara baada ya kuinuka kiuchumi.
“Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS ilifanya tathimini juu ya mpango huu,na kubaini kwamba bila TASAF kiwango cha umaskini kilichopo leo kingekuwa juu kwa asilimia 8, hivyo mchango wa TASAF ni mkubwa kwa kufanikisha niya ya Serikali kuondokana na umaskini,”amesema Kidanka.

Amesema kupitia mpango huo, Kaya nyingi zimeboresha makazi yao,uandikishaji wanafunzi umeongezeka shuleni,mahudhurio ya watoto kwenye klinik yameongezeka wenye kuanzia miezi 0-24, pamoja kuongezeka kwa matumizi ya pembe Jeo.
Amesema pia, kwa Walengwa ambao wameondoka kwenye mpango huo baada ya kuninuka kiuchumi, wameanzishiwa Ruzuku za uzalishaji kwa kuanzishwa miradi ya kibiashara,na kwamba pia kuna vikundi vimeundwa vya Akiba na kukopeshana, na kuna vikundi zaidi ya elfu 50 vimeundwa,vikiwa na wanachama 680,000, na mpaka sasa vimekusanya zaidi ya sh.bilioni 7.9, na kati ya fedha hizo bilioni 3.1 zinazunguka kwa kukopeshana.

Amesema kwa upande wa ajira za muda zimeshatolewa kwa Walengwa Laki Tano, na zaidi ya miradi milioni 27 imetolewa Tanzania bara, huku Walengwa Laki 626,000 wamefikiwa na miradi hiyo moja kwa moja, na kwamba zaidi ya sh.bilioni 110 zimeingizwa kwenye miradi hiyo.
Amesema pia wameshirikiana na Bodi ya mikopo ya elimu ya juu, na kutoa mikopo kwa watoto wa Walengwa wa TASAF kwa asilimia 100, na kwamba zaidi ya wanafunzi milioni 1 wamepata mikopo hiyo moja kwa moja.

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru, ameishukuru TASAF kwa kuendelea kushirikiana nao kwa hatua mbalimbali, pamoja na kuelimisha wananchi juu ya mpango huo.

TAZAMA PICHA👇👇
Afisa Habari na Mawasiliano kutoka TASAF Christopher Kidanka akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Greysona Kakuru akizungumza kwenye mkutano huo.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Patrick Mabula akizungumza kwenye mkutano huo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Ntuli Mwakahesya akizungumza kwenye mkutano huo.
Viongozi wakiwa Meza Kuu.
Wanachama wa SPC wakiwa kwenye mkutano.


 
Picha ya pamoja.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464