MISA TAN YAIPONGEZA TEF KWA KUFANYA UCHAGUZI SALAMA

MISA Tanzania yaipongeza TEF Kwa kufanya uchaguzi salama.

Mwandishi wetu

Dodoma

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika, Tawi la Tanzania ( MISA Tan) Bwana Edwin Soko amelipongeza jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Kwa kufanya uchaguzi wao salama na kuwapata viongozi wake watakaokuwa na dhamana ya kuingiza TEF Kwa miaka minne. .

" MISA Tan tunampongeza Mwenyekiti Deodatusi Balile na kamati yake ya utendaji Kwa kuchaguliwa tena kuiongoza TEF, hiyo ni imani kubwa Kwa wana TEF" alisema Edwin Soko Mwenyekiti wa MISA Tan.

Bwana Soko pia aliongeza kuwa, MISA Tan ina mahusiano mazuri na TEF hivyo itaendelea kufanya kazi Kwa ukaribu na TEF.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464