UVCCM(W)SHINYANGA MJINI WAPOKELEWA NA MAHABA MAKUBWA KOLANDOTO,ZIARA YA MAMA FULL BOX OPARESHENI

UVCCM(W)SHINYANGA MJINI WAPOKELEWA NA MAHABA MAKUBWA KOLANDOTO,ZIARA YA MAMA FULL BOX OPARESHENI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini,wamepokelewa na umati mkubwa wa watu katika ziara yao ya Mama Full Box Oparesheni katika Kata ya Kolandoto,na kuonyeshwa mahaba makubwa jinsi gani wananchi wa Kata hiyo waliyonayo juu ya CCM, kutokana na kazi ambazo anazifanya Rais Samia Suluhu Hassan za kuwaletea maendeleo.
Ziara hiyo ya Mama Full Box Oparesheni,ambayo inafanywa na UVCCM, ni kwa ajili ya kuwa andaa wananchi na uchaguzi mkuu 2025, pamoja na kuzindua mashina ya Mama katika Kata zote 17 za Manispaa ya Shinyanga, ambapo leo Aprili 7,2025 wamefika katika Kata ya Ibadakuli na Kolandoto.

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala, akizungumza na wananchi wa Kolandoto mara baada ya kumaliza kuzindua Shina la Mama kwenye Kata hiyo, amesema wao kama vijana wameridhishwa na kazi kubwa ambayo anaifanya Rais Samia, na ndiyo maana wanafanya ziara hiyo ili kuwa andaa wananchi na uchaguzi mkuu, pamoja na kumpigia kura nyingi Rais Samia siku ya uchaguzi Oktoba mwaka huu.
“Ziara yetu hii ya Mama Full Box Oparesheni,lengo lake ni kuwa andaa wananchi na uchaguzi mkuu 2025, pamoja na siku ya upigaji kura tunataka sanduku lijae kura za Rais Samia ili ashinde kwa kishindo, na kuendelea kuwatumikia Watanzania katika kuwaletea maendeleo,”amesema Sakala.

Amesema kuwa, katika Kata hiyo ya Kolandoto miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa, ikiwamo ya sekta ya Elimu, Afya,Umeme na Maji.
Aidha,amewataka pia vijana kwamba kipenga cha uchaguzi mkuu kitakapo tangazawa, kwamba wajitokeze kwa wigi kuchukua fomu za kugombea nafasi za Udiwani pamoja na Ubunge.

Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula, amesema kwa mapokezi makubwa ambayo wameonyesha wananchi kwa Kolandoto, kwamba hawana shaka bali kura za Rais Samia zitakuwapo za kutosha siku ya uchaguzi.
Ziara hiyo ya UVCCM, Mama Full Box Oparesheni, kesho itafanyika Kata ya Chamaguha na Kizumbi, yenye kauli mbiu isemayo, 2025# Kazi na Utu,Tunasonga Mbele.

TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizungumza.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizungumza.
Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Halima Issa akizungumza.
Katibu hamasa na chipukizi UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Samson Suleiman akizungumza.
Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew akizungumza.
Naibu Meya Mstaafu wa Manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya akizungumza.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kolandoto Yusuph Izengo akizungumza.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula (kulia)akimpongeza Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kolandoto Yusuph Izengo kwa maandalizi ya mapokezi mazuri.
Uzinduzi wa Shina la Mama Kata ya Kolandoto ukiendelea.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akipokelewa Kolandoto na kukabidhiwa Bendera ya Chama.
Mapokezi yakiendelea.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akipokelewa kwa Mahaba makubwa Kolandoto.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464