MWENYEKITI UVCCM(W)SHINYANGA MJINI ABDULAZIZ SAKALA APOKELEWA KWA KISHINDO KATA YA CHIBE, ZIARA YA MAMA FULL BOX OPARESHENI
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala, amepokelewa kwa kishindo katika Kata ya Chibe, alipowasili kuzindua Shina la Mama,pamoja na kuzungumza na vijana,wananchi na wana CCM,kuwahamasisha wajiandae na uchaguzi mkuu 2025.
Ziara hiyo imefanyika leo Aprili 6,2025 yenye ujumbe wa Mama Full Box Oparesheni, ikiwa na maana kwamba siku ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu 2025, kura za Rais Samia Suluhu Hassan zijae kwenye sanduku la kura, ili apate ushindi wa kishindo na kuendelea kuwatumikia Watanzania katika kuwaletea maendeleo.
Amesema ameshukuru kwa mapokezi makubwa kwa wananchi wa Kata ya Chibe, na kuwasihi kwamba wajiande vizuri katika uchaguzi mkuu 2025, kwa kumpigia kura nyingi Rais Samia, pamoja na kuwachagua wagombea wote wa CCM kwa nafasi ya Udiwani na Ubunge.
“Chama chetu kilimpitisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwa ndiye Mgombea pekee wa Urais atakae gombea uchaguzi Mkuu 2025 kwa tiketi ya CCM na Mgombea Mwenza Dk.Emmanuel Nchimbi,na sisi tunaunga mkono Azimio la Mkutano Mkuu, na sasa tunafanya ziara ya kuhamasisha wananchi wajiandae na uchaguzi huo,pamoja na kufungua Mashina ya Mama,”amesema Sakala.
Aidha, amewataka WanaCCM pamoja na Vijana, kwamba kipenga cha uchukuaji fomu kitakapo tangazwa, wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi ya Udiwani na Ubunge.
Katika hatua nyingine amewataka vijana wachangamkie fursa za mikopo asilimia 10 za Halmashauri, mikopo ambayo inatolewa bila riba, ili wapate kuanzisha biashara na hata kujikwamua kiuchumi.
Naye Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula, amewataka WanaCCM kwamba kwa sasa waendelee kuzingatia maadili ya chama hicho, na kutowaingilia viongozi ambao bado wapo madarakani, hadi siku Bunge na Baraza la Madiwani litakapovunjwa.
Ziara hiyo ya UVCCM Mama Full Box Oparesheni, kesho itaendelea katika Kata ya Ibadakuli na Kolandoto.
TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizungumza.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizindua Shina la Mama Kata ya Chibe.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizungumza.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akicheza wimbo wa Kisukuma Lisandare.
Wananchi wakisukuma Gari la Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala kwa kuonyesha Mahaba makubwa waliyonayo kwake na kushukuru kufika katika Kata hiyo ya Chibe na kuzindua Shina la Mama.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464