UVCCM(W)SHINYANGA MJINI WAHITIMISHA ZIARA YA MAMA FULL BOX OPARESHENI KWA KISHINDO WASISITIZA UCHAGUZI MKUU 2025 UPO PALE PALE
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Shinyanga Mjini,wamehitimisha ziara ya Mama Full Box Oparesheni,huku wakiwasihi wananchi wajiandae na uchaguzi mkuu 2025,sababu utakuwepo kwa mujibu Katiba,na wapigie kura nyingi za ushindi Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Hitimisho la ziara hiyo imefanyika leo Aprili 17,2025 katika Kata za Ibinzamata na Kitangili, pamoja na kuzindua Mashina ya Mama kwenye Kata hizo, na kisha kuzungumza na wananchi na kuwahamasisha wajiandae na uchaguzi mkuu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja huo Abdulaziz Sakala,amesema wao kama vijana wa wamewiwa na kazi kubwa ambayo ameifanya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka yake minne,na kuweletea maendeleo wananchi.
Amesema kutokana na kazi hiyo pamoja na kupitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM kuwa ndiye Mgombea pekee wa Urais 2025 kwa tiketi ya CCM, wakaamua kufanya ziara ya kuhamasisha wananchi wajiandae na uchaguzi mkuu, pamoja na kumpigia kura nyingi za ushindi Rais Samia ili aendelee kuwaongoza Mitano Tena.
"Ndugu zangu Rais Samia ndani ya miaka yake minne ya dhahabu amefanya mambo makubwa sana katika nchi hii,miradi mingi ikiwamo ya kimkakati ambayo iliachwa na Hayati Rais Magufuli ameikamilisha, likiwamo Daraja la Busisi,Reli ya SGR,Bwawa la Mwalimu Nyerere na hapa Shinyanga ujenzi Uwanja wa Ndege," amesema Sakala.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula, amesewasihi wananchi kwamba wajiandae na uchaguzi sababu utakuwepo kwa mujibu Katiba, na siku hiyo ya uchaguzi wawapigie kura wagombea wote wa CCM,kwa nafasi ya Udiwani,Ubunge na Rais.
Amesema CCM watafanya kampeni za Kistaarabu na za amani, na kuwasihi wananchi wasijiingize kwenye mtego wa Chama kimoja cha upinzani ambacho kinataka kuvuruga Amani siku ya uchaguzi mkuu,wakidai mabadiliko.
"Vijana nawasihi msije kutumika kisiasa kuvuruga amani siku ya uchaguzi mkuu, hao viongozi wa upinzani wanaotaka kuharibu uchaguzi familia zao hazipo hapa nchi,natutakao umia ni mimi na wewe ambao familia zetu zipo nchini,hivyo tuwapuuze na kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu,"amesema Katalambula.
Diwani wa Ibinzamata Ezekiel Sabo,amewapongeza vijana hao,kwa ziara yao ya kumsemea Rais Samia juu ya mambo makubwa ambayo ameyafanya ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Amesema Katika Kata hiyo ilani ya uchaguzi ya CCM imetekeleza kwa asilimia 85 ambapo miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa ikiwamo ujenzi wa masoko,na Stendi Kubwa ya Mabasi ya Mkoa.
Naye Diwani wa Kitangili Mariamu Nyangaka, amesema katika Kata hiyo ndani ya miaka minne ya Rais Samia, miradi mingi imetekelezwa ikiwamo ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja na ujenzi wa Zahanati ambayo haikuwepo.
Ziara hiyo ya UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini,Mama Full Box Oparesheni ilianza Aprili 5 na imehirimishwa leo Aprili 17,2025, kazi na Utu,Tunasonga Mbele.
TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizungumza.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizungumza.
Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Samson Suleiman akizungumza.
Diwani wa Ibinzamata Ezekiel Sabo akizungumza.
Diwani wa Kitangili Mariamu Nyangaka akizungumza.
Uziduzi wa Shina la Mama Kata ya Ibinzamata ukiendelea.
Uzinduzi wa Shina la Mama Kata ya Kitangili ukiendelea.