Kumbe ni mchawi aliyekuwa anaitesa familia yangu!
Ama kwa hakika uchawi na mambo ya kishirikina huwa yamesimika mizizi katika sehemu nyingi za Afrikam, watu wengi walisema kuwa watu walijingiza katika suala hili kwani hawakutaka maendeleo na ambapo walitaka kila mtu awe na umaskini.

Baba yetu ambaye ni marehemu alikuwa na ugomvi na jirani yetu mmoja kabla ya kifo chake na kulingana na jinsi mama alivyotuambia ni kwamba jirani yule alisema kuwa lolote ambalo tungejaribu kufanya halingefua dafu.