MAADHIMISHO WIKI YA WAZAZI YAZINDULIWA SHINYANGA,ELIMU YA MALEZI BORA KWA WATOTO KUTOLEWA

MAADHIMISHO WIKI YA WAZAZI YAZINDULIWA SHINYANGA,ELIMU YA MALEZI BORA KWA WATOTO KUTOLEWA

Na Mwandishi Wetu,SHINYANGA.

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amezindua rasmi maadhimisho ya wiki ya wazazi mkoani Shinyanga,ambayo yataambatana na utoaji wa elimu ya malezi bora kwa watoto,pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii.
Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 9,2025 katika shule ya Sekondari Bunambiyu wilayani Kishapu.


Awali Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Shinyanga Regina Ndulu akisoma taarifa ya jumuiya hiyo,amesema maadhimisho hayo yatafanyika katika halmashauri zote za mkoa huo, pamoja na kutolewa elimu ya malezi bora ya watoto,maadili,pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii.
Mwenyekiti CCM Mabala Mlolwa.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi, amesema maadhimisho hayo yatakuwa ya aina yake sababu yatatoa elimu mbalimbali kwa wananchi hasa katika masuala ya malezi na makuzi kwa watoto.


Naye Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa,akizungumza katika uzinduzi wa maadhimisho hayo,ameipongeza Jumuiya ya wazazi kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya ya kuhakikisha watoto wanalelewa katika malezi na maadili mema.
John Siagi Mwenyekiti Wazazi Mkoa.

Aidha,amempongeza pia Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa utendaji wake kazi ndani ya miaka yake minne ya utawala wake, pamoja na kuwaletea maendeleo wananchi wakiwamo na mkoa huo wa Shinyanga.


Amesema shukrani kubwa ambayo Rais Samia anapaswa kupewa na wananchi wa Shinyanga,ni kwamba siku ya uchaguzi mkuu wampigia kura nyingi za ushindi,ili ashinde kwa kishindo na kuendelea kuwatumikia Watanzania.


Katika uzinduzi huo wa maadhimisho ya wiki ya wazazi mkoani Shinyanga pamoja na mambo mengine liliambatana pia na zoezi la ukaguzi wa miradi ya maendeleo shule ya Sekondari Bunambiyu pamoja na upandaji Miti.



Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga leo Aprili 9, 2025.






















Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi akipanda mti.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464