Baada ya mke kupata kazi kamkimbia mume
Jina langu Juma, Mke wangu hakuwa na kazi yoyote lakini alikuwa tayari kahitimu kutoka katika chuo kikuu na mara nyingi alikuwa akifanya majaribio mbalimbali ya kutafuta kazi bila mafanikio.

Licha ya hayo yote, nilikuwa nampenda na kumdhamini ajabu mke wangu kwani nilikuwa tayari kumfanyia lolote. Mshahara wangu haukuwa mkubwa kwa kiwango kikubwa lakini nilikuwa najinyima ili kumfurahisha mke wangu wakati wowote ule.