VYAMA VYA USHIRIKA VYA SHAURIWA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO


Na Kareny Masasy,

Kahama

JUKWAA la ushirika la Mkoa wa Shinyanga limewakutanisha vyama vya ushirika 299 huku vikishauriwa kutumia fursa za mazao yaliyopo kuanzisha viwanda vidogo vidogo.

Jukwaa hilo limefanyika tarehe 11/04/2025 ambapo mwenyekiti wa jukwaa kwa mwaka huu ni Emanuel Nyambi kutoka chama kikuu cha Ushirika Wilaya Kahama (KACU) huku akieleza jukwaa lipo kisheria..

"Jukwaa hili limetukutanisha kueleza changamoto zinazotukabili na zinazoukabili ushirhirika ili kuzijadili kwa pamoja nakupata suluhisho"amesema Nyambi.

Mwakilishi kutoka chuo kikuu cha ushirika Moshi (MoCu) Dk Gratian Rwekaza ametoa mada juu ya fursa za ushirika kwenye soko huria katika kukuza uchumi wanachama na jamii kwa ujumla huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha.

Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Shinyanga Ibrahim Kikozi amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni ushirika hujenga ulimwengu ulio bora na vyama vimekuwa vikiwasaidia wanachama wake kupata pembejeo na viuatilifu.

Mbunge wa jimbo la Ushetu Emanuel Cherehani amesema viongozi wanatakiwa kufuata kanuni na sheria za ushirika kwani wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakishindwa kusimamia ushirika nakutoa maamuzi.

"Uwezo wa kusimamamia ushirika kama huna ndiyo unao maliza ushirika moja ya sifa ya kiongozi kutunza siri za vikao ,kuheshimiana nakutoyumbishwa kwani utajikuta unafanya maamuzi kwa maslahi ya mtu mmoja na baadaye kuwa gumzo kwenye vijiweni"amesema Cherehani.

Baadhi ya wadau waliohudhuria kwenye jukwaa hilo ambao ni Meneja wa Agricom kutoka Wilaya ya Kahama Christina Mabula amesema wao wanatoa suluhisho la kumkomboa mkulima mmoja mmoja au vikundi.

"Mpaka sasa wameweza kutoa trekta 400 kwa nchi nzima kwa kushirikiana na bodi ya pamba lengo wakulima waondokane na kilimo cha mazoea" amesema Mabula.

Nae mwakilishi wa Kampuni ya Global Leaf Geofrey Pofia amesema wamekuwa wakinunua zao la tumbaku msimu wa pili sasa na wameingia kwenye ushindani ili kulifanya zao liwe na tija.

Meneja wa benk ya Azania tawi la kagongwa wilaya ya Kahama Dismas Wangwe amesema wametoa mikopo kwa wakulima na fedha zimekwisha rejeshwa baada ya kukopwa na vyama.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464