UVCCM (W)SHINYANGA MJINI WAZINDUA SHINA LA MAMA KATA YA MJINI
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
JUMUIYA ya Umoja wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini,wamezindua Shina la Mama Kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga,huku wakiwahamasisha wananchi wajiande na uchaguzi mkuu 2025, pamoja na kumpigia kura nyingi za ushindi Rais Samia Suluhu Hassan.
Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 11,2025 ukiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Abdulaziz Sakala.
Sakala akizungumza wakati wa uzinduzi wa Shina hilo la Mama, amesema, wao vijana wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, wapo kwenye ziara ya Mama Full Box Operesheni, ambayo imelenga kuhamasisha wananchi wajiandae na uchaguzi mkuu 2025,kufungua Mashina ya Mama, na kuitangaza miradi ambayo imetekelezwa na Rais Samia ndani ya utawala wake wa miaka minne ya dhahabu.
“Vijana wa UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini,tumeridhishwa na kazi kubwa ambayo ameifanya Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwamo ya kimkakati, na kuamua kufanya ziara ya Mama Full Box Oparesheni, ili siku ya uchaguzi mkuu,kura za Rais Samia zijae kwenye sanduku la kupiga kura na ashinde kwa kishindo,”amesema Sakala.
Ametolea mfano baadhi ya miradi ya kimkakati ambayo Rais Samia ameikamilisha, ukiwamo ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR)Daraja na Busisi,Uwanja wa ndege Shinyanga,na Bwawa la Mwalimu Nyerere na sasa nchi itauza umeme nchi za jirani.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula, amewataka wananchi kwamba wajiandae na uchaguzi mkuu,sababu utakuwepo kwa mujibu wa Katiba ya Nchi na siyo takwa la chama chochote, na katika uchaguzi huo wakawachague wagombea wote wanaotokana na CCM, sababu ndiyo watawaletea maendeleo.
Diwani wa Mjini Gulamu Hafeez Mkadamu, amempongeza Rais Samia kwa utendaji wake kazi mzuri, na kwamba kwenye Kata hiyo miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa, ukiwamo ujenzi wa Soko kuu la kisasa pamoja na ukarabati wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Ziara hiyo ya Mama Full Box Oparesheni, ina kauli mbiu isemayo, Kazi na Utu,Tunasonga Mbele.
TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizungumza.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizingumza.
Diwani wa Mjini Gulum Hafeez Mkadamu akizungumza.
Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Samson Suleiman akizungumza.
Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Halima Issa akizungumza.
Uzinduzi Shila la Mama Kata ya Mjini ukiendelea.