DULA MSOMALI AISHAURI CCM JUU YA WAGOMBEA WA MKOANI MTWARA

 





Dula Msomali Mkazi wa Jimbo la Masasi Mkoani Mtwara wamekiomba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitisha wagombea wanaokubalika Ili waweze kutatua changamoto zilizopo ndani ya Jimbo hilo zikiwamo miundombinu mibovu ya barabara.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Katibu Mkuu na Mgombea Mwenza wa Chama hicho, Dk. Emanuel Nchimbi kufanya ziara katika Jimbo hilo pamoja na kusikiliza kero za wananchi.

Msomali amesema kuwa, Jimbo hilo lina changamoto lukuki ikiwemo miundombinu mibovu ya barabara, umeme, maji na huduma za matibabu, Hali inayosababisha baadhi ya wananchi wenye matatizo makubwa kupewa rufaa Ndanda Hospitali ambayo ipo umbali mrefu.

Amesema kuwa, idadi kubwa ya wananchi wa Masasi ni maskini, wanategemeq zaidi kilimo Cha korosho na ufuta ikiwa miundombinu ya barabara itaboreshwa wataweza kusafirisha mazao Yao na kujipatia kipato ambacho kitawasaidia kuwaondoa kwenye umaskini.

"Wananchi tunaamini chama ni siku, hivyo basi tunaiomba tupewe wagombea wanaoweza kuleta maendeleo yetu na kutuondoa kwenye umaskini 
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464