
Oparesheni Ofisa wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Emmanuel Christian Gariyamoshi, amefariki dunia Aprili 9, 2025, majira ya saa tano asubuhi akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni Ndanda iliyopo Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jeshi la Polisi, mwili wa marehemu utasafirishwa na mazishi yatafanyika nyumbani kwao katika Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma.
Kabla ya kupangiwa kazi mkoani Mtwara, ACP Gariyamoshi aliwahi kuwa Oparesheni Ofisa wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, na pia alitumikia kama Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) ya Kishapu katika mkoa huo huo wa Shinyanga.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464