UVCCM WAMKARIBISHA EMMANUEL NTOBI CCM,ZIARA YA MAMA FULL BOX OPARESHENI
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Shinyanga mjini,wamemkaribisha aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi kujiunga na CCM,ambaye alivuliwa vyazifa hiyo na Chama chake.
Hayo yamebainishwa leo Aprili 13,2025 na Jumuiya hiyo wakati wa uzinduzi wa Shina la Mama Kata ya Ngokolo,katika ziara ya Mama Full Box Oparesheni,ambapo pia walizindua Shina la Mama Kata ya Kambarage.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula,amesema wanamkaribisha Emmanuel Ntobi, kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM),kutokana na chama chake kutokuwa na uelekeo,na kwamba watampatia cheo cha Katibu Hamasa Tawi la Mwadui.
"Emmanuel Ntobi amefukuzwa na Chadema,na sisi tupo tayari kumpokea,mpelekeeni ujumbe huu,na tutampatia cheo cha Katibu Hamasa Tawi la Mwadui," amesema Katalambula.
Aidha,amewaambia wananchi kwamba uchaguzi mkuu 2025 utakuwepo na hakuna mtu ambaye wala chama chochote kinaweza kuzuia uchaguzi huo, sababu ni takwa la kikatiba.
Amesema hapa nchini kuna vyama 19 vya siasa, na vyama 18 vimekubali kushiriki kwenye uchaguzi mkuu,kasoro chama kimoja cha Chadema,na kwamba aliyesusa uchaguzi asuse na uchaguzi upo pale pale kwa mujibu wa Katiba ya Nchi.
Mwenyekiti wa (UVCCM)wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala, amesema Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) kipo tayari kushiriki kwenye uchaguzi mkuu,ambapo tayari kimeshampitisha Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM kwenye uchaguzi huo.
Amewasihi pia vijana wasiwe tayari kutumika kisiasa kuvuruga amani ,sababu ya chama kimoja kutokuwa tayari kushiriki uchaguzi mkuu, na kimelenga kuchafua amani ya nchi.
"Wenzetu wa Chadema hawapo tayari kushiriki uchaguzi mkuu na jana mmeona wamegoma kusaini kanuni za maadili,na hawapo tayari kwa maridhiano, na lengo lao ni kuvuruga amani, hivyo nawaomba vijana msikubali kutumika kuvuruga amani,bali tuilinde amani ya nchi yetu kwa nguvu zote," amesema Sakala.
Ziara hiyo ya Mama Full Box Oparesheni,lengo lake ni kuhamasisha wananchi wajiandae na uchaguzi mkuu 2025,pamoja na siku ya uchaguzi wampigie kura nyingi za ushindi Rais Samia,na kujaza sanduku la kura ili ashinde kwa kishindo.
TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala akizungumza.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizungumza.
Katibu Hamasa na Chipukizi UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Samson Suleiman akizungumza.
Diwani wa Ngokolo Victor Mkwizu akizungumza.
Diwani wa Kambarage Hassan Mwendapole akizungumza.
Uzinduzi Shina la Mama Kata ya Kambarage ukiendelea.
Uzinduzi Shina la Mama Kata ya Ngokolo ukiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464